PCs and QT notification


 PRIVATE  CANDIDATE AND  QT   NOTIFICATION



education  blog  ingependa   kuwakumbusha    watahiniwa   wa  mitihani  ya  kujitegemea PCs  kuhakiki   taarifa   zao  kabla  ya kuingia  chumba  cha mtihani.  
taarifa  hizo  ni barua   ya  uthibitisho  kutoka baraza  la mitihani tanzania (NECTA) ikiwa  ina taarifa za kumruhusu  mwanafunzi kufanya  mitihani fulani.    kawaida   barua  hizo huambatanishwa na:

1. jina la mwanafunzi
2. picha
3. namba ya mtihani
4. muda wa mtihani
5. kituo cha mtihani
n.k

masomo  atayofanya  mwanafunzi  yataonekana    kama  ifuatavyo:







barua hiyo  itaweza  kuonekana  kama  ifuatavyo:




taarifa hizi  mwanafunzi  yapasa  azihakiki  kama ni sahihi,  kama vile herufi za jina lake pamoja  na mitihani   aliyochagua  kufanya.

education blog  ingependa   kuwasihi   wanafunzi  wa  QT  kufanya  mazoezi   zaidi katika  kuandika, ukizingatia  mitihani yao itafanyika   ndani  ya masaa  matatu tu.  kwa  masomo  matano

wanafunzi wa private candidate kufanya   mazoezi   zaidi  katika  uandishi  wa insha za kiswahili  na  kingereza   ukizingatia  ni vipengere  vyenye  alama  nyingi.

MAKOSA  KATIKA  CHUMBA  CHA MTIHANI

si  ruhusa  kufanya udanganyifu wowote  katika  chumba cha mtihani,  kufanya hivyo ni kosa kisheria,   waweza kushtakiwa au  kufungiwa  kabisa  kutofanya mitihani ya necta kwa miaka kadhaa.


wanafunzi  wanashauriwa  kufanya juhudi  binafsi,  hii itawajengea  uwezo  hata wakifika  kwenye  elimu za  juu 


   maandalizi  mema  ya mitihani  2015