MBINU ZA KUFUNDISHA


                                                    MBINU ZA KUFUNDISHA



Uchaguzi bora wa Mbinu na Njia za Kufundishia


Mbinu na Njia za Kufundishia

Ni Jumla ya vitendo vya maandalizi ya somo linalokusudiwa, matumizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, vitendo vya mwanafunzi katika harakati za kujifunza na jukumu la Mwalimu kinadharia na vitendo katika ufundishaji na ujifunzaji.
Maana ya Mbinu za Kufundishia
Ni mwongozo mbalimbali atumiao Mwalimu darasani wakati wa kuwasilisha somo alilioliandaa kwa wanafunzi wake.
Mwalimu anapashwa kuaamua kwa kuchagua kwa makini Njia na Mbinu bora za kufundishia ili wanafunzi wake waweze kujifunza kwa ufanisi.
Misingi ya kuchagua njia na mbinu ni kuzingatia mambo yafuatayo:-
Maudhui ya somo.
  • Mwalimu lazima azingatie hali ya somo, maarifa na stadi anayopaswa kujenga mwanafunzi.
Hali  na umri wa wanafunzi wako.
  • Mwalimu lazima azingatie umri wa wanafunzi, kukomaa au kutokomaa kwa akili za wanafunzi na mazingira yao ya nyumbani na ya shuleni.
Malengo ya somo.
  • Bainisha mambo ambayo wanafunzi wako wanataka kufanikisha katika maisha yao.
Uwezo wa Mwalimu juu ya somo au mada husika.
  • Zingatia uwezo wako, ujuzi, utaalamu ulionao katika kutumia mbinu au njia inayotarajiwa.
Vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Zingatia upatikanaji wa zana na vifaa shuleni au katika mazingira ya shule (Zingatia ufaraguzi wa Zana).
Vionjo na hali ya wanafunzi.
  • Njia au mbinu utakazotumia zioane na vionjo na hali za wanafunzi. Njia zisipingane na sifa hizo kwani malengo ya somo hayawezi kufanikisha