
Sura
Madhumuni
Utangulizi
wa
Stadi za
Maisha
• Orodhesha
tabia hatarishi wanazokutana nazo vijana katika jamii
• Tambulisha
stadi za maisha ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kupunguza
hatari na
kujenga maisha ya kiafya ya baadae
• Orodhesha aina nne za stadi za maisha
2
Stadi za
Hisia
• Kuelewa
maana ya misamiati ya kujiheshimu na kujiamini
• Kuoanisha
kiwango cha mtu cha kujiheshimu
• Kufikiri
jinsi ya kuboresha afya ya kihisia ya mtu binafsi
3
Stadi za
Mawasiliano
• Tambua umuhimu wa mawasiliano ya vitendo
• Elewa mawasiliano ya tabia za ugomvi, utulivu na msimamo
• Elewa na fanya mazoezi ya kufuata hatua za kufanya mwitiko wa tabia ya
msimamo
• Tambua mbinu za kushawishi na namna ya kukabiliana nazo
4
Kufanya
Maamuzi
• Tambua
umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi
• Eleza
hatua zinazotumika kufanya maamuzi sahihi
5
Mapenzi na
Mahusiano
• Elewa
umuhimu wa urafiki
• Tambua
shinikizo rika na fikiria jinsi mtu anavyoweza kupambana nao
• Fikiria
kuhusu mapenzi na umuhimu katika uhusiano wa kimapenzi
6
Ngono ya
Kulazimishwa
• Kubainisha
kwamba ngono ya kulazimishwa hutokea na ni hatari
• Kugundua
hali ambazo ngono ya kulazimishwa inaweza kutokea
• Fikiria
kuhusu njia ambazo mtu anaweza kujikinga mwenyewe
7
Majukumu
ya
Kijinsia
• Kueleza
maana ya “majukumu ya kijinsia”
• Kueleza
tofauti kati ya “jinsi” na “majukumu ya kijinsia”
• Kuorodhesha
majukumu yanayotarajiwa kwa wanaume na wanawake katika
jamii
• Kueleza
changamoto kwa majukumu ya sasa ya kijinsia na jinsi
yanavyoweza
kubadilishwa katika hii jamii
8
Ndoto na
Malengo
• Kufikiria
kuhusu malengo na tamaa zao
• Kugundua
kwamba kupanga na kufanya vitendo kunahitajika kufanya ndoto
na malengo
kutokea
Wenye Elimu Ndogo
Kila kikundi cha vijana
ni tofauti. Ni muhimu muwezeshaji achukue muda wa
kutathmini mahitaji ya
kikundi ili njia bora zinazofaa za kukidhi mahitaji hayo ziweze
kutumiwa. Ili kutumia
mazoezi yaliyo kwenye kitabu hiki kwa ajili ya vijana wenye
uzoefu mdogo wa kusoma
na kuandika, fuata kanuni na mwongozo hapo chini.
Kanuni za Msing
:
Kuwa mbunifu: unaweza kutafuta njia za kuchekesha na za kuvutia ili kutekeleza
zoezi hilo hilo au zoezi jipya kabisa
kufanikisha malengo.
Shirikisha kikundi:
Washirikishe washiriki mara nyingi iwezekanavyo
kukusaidia
katika maandalizi yoyote yanayohitaji kufanyika,
pamoja na kutayarisha chumba,
kuandaa zana za kazi n.k.
UTANGULIZI
Mwongozo wa Stadi za Mpango wa Maisha Tanzania
9
Tumia vielelezo vya kuona na kusikisia
kadri iwezekanavyo. Hii ni pamoja na
mabango, picha, michoro, mifano na zana nyingine za
kienyeji zitakazotajwa na
kikundi n.k.
Miongozo:
_ Tumia lugha rahisi na ya wenyeji pamoja na istilahi
rahisi zinazojulikana kadri
iwezekanavyo.
_ Tumia kazi za vikundi na kuwashirikisha zaidi.
_ Waache wanakikundi wajibu maswali na watoe muhtasari
kadri iwezekanavyo
kwa kutumia lugha zao za makabila na istilahi zao.
_ Tumia mifano halisi ya maisha unapojaribu kutoa hoja
ya kweli.
_ Tumia vitu vya kawaida na vya kila siku kama sehemu ya nyenzo za
kufundishia pale inapowezekana kwa mfano, karatasi,
makopo, vifungo, vijiti
n.k. Hakikisha kikundi kinakusanya vitu hivi pindi
vikihitajika.
_ Mwulize mtu mmoja katika kikundi arudie au anakili
kile ulichosema au
ulichofanya ili kuhakikisha kwamba kikundi kinaelewa.
_ Tumia vitendo vitakavyowashirikisha vijana kama vile:
· Kucheza michezo; michezo ya
karata ni mizuri. Hii inaweza kuhitaji
kutayarishwa kuanzia mwanzo kabisa kutegemeana na
jambo lenyewe.
Achia kikundi kisaidie kama
inawezekana, kwa kuwaruhusu:
o kiainishe zoezi
o kikusanye na kukata picha
o kikate au kubandika kadi
· Kutengeneza vigandisho (picha zitengenezwazo kwa
kukata vipande
vidogo vya karatasi na kuvibandika kwenye mbao au
kiegemeo chochote
kigumu).
· Kutunga nyimbo na mashairi kwa kutumia taarifa za
kweli. Hii inasaidia
kuzikumbuka taarifa za kweli kirahisi, hasa kama washiriki watakuwa
wametunga nyimbo zao wenyewe na mashairi yao na kukifundisha
kikundi.
_ Wahimize na kuwaruhusu wanakikundi kuchangia uzoefu
wao ili waweze
kujifunza kutoka kwa kila mtu.
_ Tumia sanaa ya jadi, hadithi na methali zinazohusiana
na uzoefu wa maisha ya
kujenga maadili, kufundisha na kujifunza.
_ Wahimize kwa mifano ya maonyesho pale inapowezekana.
Uongozwe na
mahitaji ya kikundi.